Mwongozo Wa Hiari Kuhusu Uwajibikaji Katika Usimamizi Wa Umiliki Wa Ardhi, Maeneo Ya Uvuvi Na Misitu Kwa Ajili Ya Upatikanaji Na Uhakika Wa Chakula Kwa Taifa

Mwongozo huu ni nyenzo ya kwanza yenye kina na ya kimataifa kuhusu usimamizi wa umiliki iliyoandaliwa kupitia mashauriano ya kiserikali. Ndani mwake mna ufafanuzi wa kanuni na viwango vilivyokubalika kimataifa kuhusu vitendo vyenye uwajibikaji katika matumizi na udhibiti wa ardhi, maeneo ya uvuvi na misitu. Kanuni zilizomo zinatoa mwelekeo wa kuimarisha sera, sheria na taratibu za kiasasi zinazodhibiti haki za umiliki; uendelezaji wenye uwazi na usimamizi bora wa mifumo wa miliki; na kuimarisha uwezo na utendaji kazi wa mashirika ya umma, mashirika binafsi ya uwekezaji, asasi za kiraia, na watu wenye maslahi katika umiliki na usimamizi wa miliki. Miongozo iliyomo humu imejadili usimamizi wa umiliki katika kiwango cha kitaifa kwa ajili ya upatikanaji wa chakula kwa uhakika, na imekusudiwa kuchangia katika upatikanaji, kwa hatua, wa chakula cha kutosha, kutokomeza umaskini, kulinda mazingira na kufanikisha maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.

Saved in:
Bibliographic Details
Main Author: FAO
Format: Book (stand-alone) biblioteca
Language:Swahili
Published: FAO ; 2021
Online Access:https://openknowledge.fao.org/handle/20.500.14283/I2801SW
http://www.fao.org/3/i2801sw/i2801sw.pdf
Tags: Add Tag
No Tags, Be the first to tag this record!